Viongozi wa ODM walivyojumuika na wasanii wa bongo (picha)


– Ali Kiba alitumbuiza mashabiki wakati wa kusherehekea miaka 10 baada ya kuundwa kwa ODM Mombasa Baada ya kuwatumbuiza mashabiki wa ODM wakati wa kuadhimisha miaka 10 baada ya kuundwa kwa chama hicho, Ali Kiba alipata kiamsha kinywa akiandamana na magavana kadhaa asubuhi iliyofuatia.


Tukio hilo lilitokea wakati ambapo mwimbaji mwenzake kutoka Tanzania Diamond Platinums alikuwa ameondoka Mombasa.
Diamond wakati wa sherehe za ODM
ODM ilifanya sherehe hizo wakati chama kipya cha Jubilee kilikuwa kikizinduliwa katika Uwanja wa Kasarani Jumamosi Septemba 10
Kulingana na tetesi, Ali Kiba alipokea shilingi milioni nne ilhali Diamond alipokea shilingi milioni tano.
Hata hivyo Wakenya walikosoa ODM kulingana na jinsi ilivyowalipa waimbaji kutoka Kenya kwa kusema baadhi yao walipata Sh 100,000 na wengine Sh 80,000

Related Posts